Upatikanaji viungo

Breaking News
Ijumaa, Aprili 19, 2024 Local time: 00:30

Gaidi ahukumiwa maisha jela


Taswira ya Faisal Shahzad aliyejaribu kulipua mabomu huko Times Square, Ny
Taswira ya Faisal Shahzad aliyejaribu kulipua mabomu huko Times Square, Ny

M’marekani mwenye asili ya Pakistan, aliyejaza milipuko kwenye gari katika mtaa wa Times Square, mjini New York mwezi Mei mwaka uliopita amehukumiwa kwenda jela maisha.

M’marekani mwenye asili ya Pakistan, aliyejaza milipuko kwenye gari katika mtaa wa Times Square, mjini New York mwezi Mei mwaka uliopita, akitaraji kuuwa idadi kubwa ya watu, amehukumiwa kifungo cha maisha jela bila uwezekano wa kuachiwa huru.

Chumba cha mahakama kilokuwa kimejaa watu, kilikuwa kimya pale Faisal Shahzad alipoingizwa na askari kusikiliza hukumu yake kwa mashitaka 10 ya uhalifu ambayo tayari alikuwa amekiri hapo mwezi Juni.

Jaji Miriam Goldman Cedarbaum alimpatia Shahzad nafasi ya kutoa taarifa kabla hajamhukumu.

Shahzad alimwambia jaji huyo kuwa hukumu yake haimaanishi chochote kwake, na akiuliza “ Mahakama hii inawezaje kunihukumu mimi bila kufahamu mateso ya watu wangu?” Aliendelea kumwambia jaji huyo kuwa anatabiri kwamba atakwenda ahera wakati Allah atakapo mhukumu yeye.

Shahzad ambaye anakiri kuwa ana msimamo mkali wa kidini, Aliikosoa Marekani kwa juhudi zake za kijeshi za kuleta demokrasia na uhuru nchini Iraq na Afghanistan, na akawaonya wamarekani ‘watahadhari’. Jaji Cedarbaum hakutetereka. Alimhukumu kifungo cha maisha jela pasipo uwezekano wa kutoka, na akasema kabla Shahzad kuondolewa mahakamani kuwa anataraji kuwa Shahzad atatumia muda wake jela kutafakari ikiwa Quran kweli ilimtaka auwe watu.

XS
SM
MD
LG