Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumapili, Septemba 25, 2022 Local time: 01:18

Ban Ki Moon awataka wagombea urais nchini Gabon kutojitangazia ushindi.


Katibu mkuu wa umoja wa mataifa Ban Ki- Moon

Katibu mkuu wa Umoja wa mataifa Ban Ki Moon amewataka wagombea urais nchini Gabon kutojitangazia ushindi katika uchaguzi wa Jumamosi mpaka matokeo rasmi yatangazwe.

Mgombea wa upinzani Jean Ping amesema Jumapili kwamba matokeo ya waswali yanaonyesha kuwa ameshinda uchaguzi wakati msemaji wa rais aliyepo madarakani Ali Bongo amesema rais anaelekea kwenye muhula wa pili.

Gabon haina mfumo wa uchaguzi wa duru ya pili kwa hiyo mgombea mwenye kura nyingi zaidi kati ya 10 waliopo ndiye atakuwa mshindi. Ikiwa Ping kiongozi wa zamani wa umoja wa Afrika atashinda itakuwa ndio mwisho wa utawala wa familia ya Bongo uliodumu kwa nusu karne. Ali Bongo alimrithi madaraka baba yake Omar Bongo ambaye aliongoza nchi hiyo kwa zaidi ya miaka 40.

Facebook Forum

XS
SM
MD
LG