Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumanne, Mei 28, 2024 Local time: 04:04

Upinzani wa Gabon wafikisha mashtaka mahakamani


Ghasia zilizotokea mjini Libreville, Gabon baada ya uchaguzi kutangazwa.
Ghasia zilizotokea mjini Libreville, Gabon baada ya uchaguzi kutangazwa.

Mwakilishi wa koingozi wa upinzani nchini Gabon,Jean Ping, amesema kiongozi huyo amewasilisha mashtaka rasmi mbele ya mahakama.

Mwakilishi wa koingozi wa upinzani nchini Gabon,Jean Ping, amesema kiongozi huyo amewasilisha mashtaka rasmi mbele ya mahakama ili kupinga matokeo uchaguzi wa rais uliofanyika agosti 27 mwaka huu kutokana na shinikizo kutoka kwa jumwiya ya kimataifa.

Paul Marie Gondjout amesema miongoni mwa viongozi waliomshinikiza kuchukua hatua hiyo ni katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa.

Godjout ameambia VOA kwamba Ban ki-moon pamoja na waziri wa mambo ya nje wa Ufaransa Jean Marc Ayraut walimuomba Ping kuwasilisha mashtaka yake mbele ya Mahakama ya kikatiba.

Amesema kuwa wanataka jamii ya kimataifa kuingilia hali ya kisiasa nchini humo kwa kuwa inaweza kua mbaya zaidi kama hatua za haraka hazitachukuliwa.

XS
SM
MD
LG