Upatikanaji viungo

Breaking News
Ijumaa, Juni 21, 2024 Local time: 20:23

Ali Bongo aapishwa kuwa Rais wa Gabon


Rais Ali Bongo Ondimba wa Gabon.
Rais Ali Bongo Ondimba wa Gabon.

Ali Bongo Ondimba ameapishwa tena kama Rais wa Gabon kwa mhula mwingine wa miaka saba.

Ali Bongo Ondimba Jumatano ameapishwa tena kama Rais wa Gabon kwa mhula mwingine wa miaka 7 baada ya kushinda kwa kura chache kwenye uchaguzi uliogubikwa na utata.

Ushindi wa Bongo wa chini ya kura 6,000 ulisababisha ghasia na maandamano kote nchini baada ya matokeo ya awali kutangazwa Agosti 27. Takriban watu 6 waliuwawa kwenye mapambano kati ya waandamanaji na vikosi vya usalama.

Mahakama ya katiba nchini humo Jumamosi ilitupilia mbali ombi la mgombea wa upinazani Jean Ping la kutaka kuhesabiwa tena kwa kura na kuidhinisha matokeo.

Uchaguzi huo wenye utata umevutia uangalizi wa kimataifa kwa Rais Bongo ambae familia yake imetawala taifa hilo la Afrika ya kati lenye utajiri wa mafuta kwa miaka 49

XS
SM
MD
LG