Upatikanaji viungo

Breaking News
Alhamisi, Desemba 05, 2024 Local time: 17:18

G7 wametangaza msaada wa dhati kupambana na Russia na kujenga Ukraine


Viongozi wa nchi saba zenye nguvu kubwa duniani G7 katika mkutano ambao pia ulihudhuria na rais wa Ukraine Volodymyr Zelenziky kwa njia ya video
Viongozi wa nchi saba zenye nguvu kubwa duniani G7 katika mkutano ambao pia ulihudhuria na rais wa Ukraine Volodymyr Zelenziky kwa njia ya video

Viongozi wa nchi saba wametangaza msaada wao wa dhati usiotetereka na wenye mshikamano kwa Ukraine ikiwemo wa mahitaji ya haraka ya kijeshi na vifaa vya ulinzi ili kuendelea kupambana na uvamizi wa Russia.

Taarifa iliyotolewa na White house inasema kwamba nchi 7 tajiri zaidi duniani zimekemea hatua ya Russia kuendelea kuishambulia Ukraine na kusababisha hali mbaya ya kibinadamu kwa kulenga mifumo muhimu hasa nshati na maji katika miji kadhaa ya Ukraine.

Nchi hizo zimeyataja mashambulizi hayo holela kuwa uhalifu wa kivita na kuwashutumu wanaofanikisha vita vya Putin nchini Ukraine wanavyosema vinatekelezwa kinyume cha sheria.

Taarifa hiyo imetolewa siku moja kabla ya kongamano la nchi saba tajiri duniani G7, litakalofanyika mjini Paris, Ufaransa, na lenye lengo la kupanga namna ya kuijenga upya Ukraine.

Rais wa Ukraine Volodymyr Zelenskyy amehudhuria mkutano kwa njia ya video. Kansela wa Ujerumani Olaf Scholz, ambaye ndiye rais wa muungano wa G7, amesema watahakikisha kwamba uchumi wa Ukraine unaimarika n akuijenga upya nchi hiyo kutumia mpango uliotumiwa na Marekani kujenga upya ulaya baada ya vita vya pili vya dunia.

XS
SM
MD
LG