Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatano, Juni 07, 2023 Local time: 02:19

G20 Zaahidi Kupunguza Nakisi za Bajeti


Nchi za kundi la G20 zinazokutana Canada zimekubaliana kuhakikisha nchi tajiri zinapunguza nakisi za bajeti zao.

Viongozi wa mataifa ya kundi la G20 waliokutana Toronto, Canada, wamekubaliana kuwa nchi zenye utajiri mkubwa wa viwanda hazina budi kupunguza nakisi za bajeti zao kwa nusu nzima katika muda wa miaka mitatu, na kuchukua hatua zaidi za kupunguza madeni kulinganisha na uzalishaji wa kiuchumi ifikapo 2016.

Mataifa ya G20, ikiwa ni pamoja na mataifa makubwa ya viwanda katika kundi la G8 pamoja na nchi zinazoendelea ambazo zina uchumi mzuri kama vile China na India, zimekubaliana muda maalum wa kupunguza nakisi za bajeti, huku zikitoa uwezo kwa serikali kurekebisha mwendo wao wa mabadiliko kulingana na hali halisi katika nchi zao.

Mpango uliodhaminiwa na mwenyeji wa mkutano, Canada, utazitaka nchi matajiri kupunguza mapungufu yao katika bajeti kwa nusu nzima ifikapo mwaka 2013. Ifikapo 2016, serikali zitatakiwa kuanza kupunguza asilimia ya madeni kwa kulinganisha na pato la uzalishaji wa taifa, thamani ya biadhaa na huduma zinazotolewa nchini humo.

XS
SM
MD
LG