Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumamosi, Oktoba 05, 2024 Local time: 03:25

DRC yalalamika baada ya kushambuliwa rais wa Senet mjini Paris


Rais wa Baraza la S$enet la Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo leon Kengo Wa Dondo akizungumza na waandishi habari.
Rais wa Baraza la S$enet la Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo leon Kengo Wa Dondo akizungumza na waandishi habari.

Serikali ya Ufaransa inawasaka waliohusika kwa shambulizi la kiongozi mmoja wa serikali ya DRC akiwa mjini Paris

Maafisa wa usalama huko Ufaransa wanawasaka watuhumiwa waliohusika katika shambulizi dhidi ya rais wa baraza la Senet la Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo-DRC, Leon Kengo Wa Dondo mjini Paris.

Ripoti kutoka Paris zinasema kwamba wakuu wa serikali ya Congo wamewasilisha rasmi malalamiko yao kutokana na tukio hilo wakidai Ufaransa haikuchukua hatua za kutosha kukabiliana na tukio hilo.

Kufuatana na ripoti hiyo ni kwamba maafisa wa usalama wanasema wanafanya kila wawezalo kuwasaka waliomshambulia rais wa baraza la senet la Congo, Wa Dondo, wakati alipokua anashuka kutoka kituo kimoja cha treni mjini Paris. Hivi sasa bwana Kengo anapatiwa matibabu katika hospitali moja mjini Paris.

Hata hivyo wakuu wa Congo walimuita balozi wa Ufaransa mjini Kinshasa, kumhoji juu ya tukio hilo. Wanasema ilibidi serikali ya Paris impatie usalama bwana Kengo, ingawa wakuu wa Ufaransa wanasema hawakuarifiwa juu ya ziara hiyo, kwa wakati unaostahiki.

Akizungumza na televisheni moja ya Ufaransa, waziri wa habari wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, Lambert Mende, anasema Ufaransa haikulishughulikia suala hilo vilivyo.

Chama kikuu cha upinzani nchini Congo, Union for Democracy and Social Progress-UDSP, kimejitenga na tukio hilo dhidi ya Kengo.

Shambulio la Paris lilitokea wiki chache tu baada ya ugomvi kufuatia uchaguzi wa rais nchini Congo ambao ulikuwa na utata.Kiongozi wa UDPS, Etienne Tshisekedi, anadai kulikuwa na wizi wa kura uliompatia ushindi Rais Joseph Kabila.

Ufaransa na ubelgiji, ambao ni utawala wa zamani wa kikoloni umetoa hoja juu ya matokeo hayo ya uchaguzi wa rais na Marekani na makundi ya kutetea haki wameeleza kuwa kulikuwepo na kasoro nyingi kwenye utaratibu wa uchaguzi.






XS
SM
MD
LG