Wine ambaye jina lake halisi ni Robert Kyagulanyi Ssentamu alikuwa mpinzani mkubwa katika uchaguzi wa mwaka 2021 wa rais aliyoko madarakani kwa muda mrefu nchini Uganda, Yoweri Museveni aliyeshinda kwa asilimia 58 ya kura.
"siku zote nimekuwa nikitaka mambo yabadilike. Na hata katika muziki wangu wote nilikuwa nikiimba kuhusu mabadiliko chanya, mabadiliko ya tabia, Fikiria za VVU, UKIMWI, usafi wa mazingira na haya yote. Lakini kama miaka 15 iliyopita, nilivamiwa na maafisa wa usalama na kupigwa kwasababu tu nilikuwa na gari zuri na wasichana walikuwa wakinirushia mabusu , nilikuwa kijana mdogo. Alinichapa kofi na kuniuliza kwanini nilikuwa najionyesha , kama vile sikujua kwamba nchi ilikuwa na wamiliki. Hiyo ilinipa changamoto kukumbuka kwamba watu wengi wamepitia na bado wanapitia mambo hayo. Lakini nilikuwa najiamini kufikiria kwamba nilikuwa salama. Hapo ndipo niligundua kwamba hakuna aliye salama katika vita hivi. Ndipo nilibadili mtindo wangu wa muziki. Hata hivyo baada ya miaka mingine 10 ya kuimba muziki mzuri na unaozingatia siasa bado hali haikubadilika sana kwa hiyo niliamua kuchukua hatua na kuingia katika siasa ili kuona kwamba hii kweli inabadilika.”