Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumapili, Julai 14, 2024 Local time: 22:15

Timu nyingine ya Afrika yaanguka Russia 2018


Wachezaji wa Uingereza wakishangilia goli la Harry Kane dhidi ya Tunisia 18 Juni 2018.
Wachezaji wa Uingereza wakishangilia goli la Harry Kane dhidi ya Tunisia 18 Juni 2018.

Timu nyingine ya Afrika imepoteza mechi yake ya ufunguzi katika fainali za kombe dunia Russia baada ya Tunisia kufungwa 2-1 na Uingereza katika mechi za Kundi G Jumatatu.

Nyota wa Uingereza Harry Kane aliipatia Uingereza mabao yote mawili, la kwanza katika dakika ya 11 ya mchezo baada ya mashambulizi makali katka lango la Tunisia.

Baada ya msukosuko wa awali Tunisia ilionekana kutulia katika mechi na kupambana vikali na Uingereza kwa kujibu mashambulizi na kutawala katikati ya uwanja kwa muda mrefu.

Tunisia ilipata penalti katika dakika ya 35 na Ferjani Sassi akatumbukiza mpira kimiani na kufanya timu hizo kwenda mapumziko zikiwa sare 1-1.

Uingereza ilionekana kuwazidi Tunisia katika kipindi cha pili lakini walinzi wa Tunisia walifanya kazi kubwa kuhimili mashambulizi. Hata hivyo, katika dakika za nyongeza Harry Kane kwa mara nyingine alipenya nyuma ya ukuta wa Tunisia na kufunga bao la kichwa kuipitia Uingereza ushindi wa 2-1.

Misri, Nigeria na Morocco zote zilipoteza mechi zao za ufunguzi tangu kuanza kwa fainali hizo wiki iliyopita. Senegal inacheza mechi yake ya kwanza Jumanne dhidi ya Poland.

XS
SM
MD
LG