Upatikanaji viungo

Breaking News
Alhamisi, Machi 28, 2024 Local time: 17:25

Rais Felix Tshisekedi kufanya ziara mjini Washington Dc


Rais wa Jamhuri ya kidemokrasia ya Congo Kinshasa,Felix Tshisekedi akiwa kwenye Umoja wa Afrika Machi 18, 2019.
Rais wa Jamhuri ya kidemokrasia ya Congo Kinshasa,Felix Tshisekedi akiwa kwenye Umoja wa Afrika Machi 18, 2019.

Suala la kupambana na mlipuko wa ugonjwa wa Ebola mashariki mwa jamhuri ya kidemokrasia ya Congo litakuwa moja ya mambo yatakayojadiliwa.

Rais wa Jamhuri ya kidemokrasia ya Congo Felix Tshisekedi atafanya ziara mjini Washington Dc mapema mwezi Aprili kujadili kuimarisha uchumi na usalama wizara ya mambo ya nje ya Marekani imeeleza Jumanne.

Msemaji Robert Palladino amesema Tshisekedi atatembelea Washington tarehe 3 hadi 5 mwezi Aprili na kufanya mikutano na waziri wa mambo ya nje Mike Pompeo pamoja na maafisa wengine wa juu wa utawala wa Trump.

Haijajulikana mara moja kama atakutana na rais Donald Trump.

“Tunaungana na matakwa ya rais Tshisekedi ya kutaka kujenga uhusiano thabiti kati ya Marekani na Jamhuri ya kidemokrasia ya Congo” Palladino aliwaambia waandishi wa habari.

Amesema suala la kupambana na mlipuko wa ugonjwa wa Ebola mashariki mwa jamhuri ya kidemokrasia ya Congo kulikogubikwa na vita litakuwa ni moja ya mambo yatakayojadiliwa.

Imetayarishwa na Sunday Shomari.

XS
SM
MD
LG