Upatikanaji viungo

Breaking News
Ijumaa, Aprili 19, 2024 Local time: 19:22

FBI haitopendekeza kufunguliwa mashtaka dhidi ya Clinton


Hillary Clinton
Hillary Clinton

Akizungumza mjini Washington siku ya Jumanne, mkurugenzi wa FBI amesema uchaguzi umekamilika na kwamba wachunguzi hawajagundua ushahidi wowote kwamba Bi Clinton alifuta barua yeyote pepe inayohusiana na kazi zake kwa makusudi.

Lakini aliongeza kusema kwamba Clinton na washauri wake hawakua waangalifu kuhusiana na habari muhimu za siri.

Mkurugenzi wa FBI, James Comey
Mkurugenzi wa FBI, James Comey

Bw Comey amesema Clinton alitumia mitambo kadhaa tofauti ya mtandao na vipakatilishi kwa ajili ya barua pepe zake binafsi na kikazi. Amesema, FBI imesoma barua zote elfu 30 katika uchunguzi wake.

Comey anasema waliamua kwamba barua pepe 110 kati ya barua pepe zilizopangwa katika makundi 52 zilikua za siri wakati zilipotumwa, na kwamba ni barua 8 tu zilikua na habari za siri ya juu kabisa ya taifa.

Comey anasema kunauwezekano maadui waliweza kuingia katika akaunti ya barua pepe ya Bi Clinton lakini hakuna madhara yaliyoonekana na kwamba ingawa kuna ushahidi ya ukiukaji wa kutumia vyombo hivyo nama alivyofanya lakini kwa uwamuzi wao hawadhani kuna “mwendesha mashtaka yeyote mwenye busara ataweza kumfungulia mashtaka”.

Mpinzani wa Bi Clinton katika uchaguzi wa rais Mrepublican Donald trump amejibu akisema ni uwamuzi usio wa haki kamwe.

XS
SM
MD
LG