Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumanne, Februari 27, 2024 Local time: 02:20

Mkuu wa FBI Marekani kuhojiwa na wabunge

James Comey
James Comey

Comey ameitwa kutoa ushahidi bungeni kwenye kamati ya bunge ya usimamizi wa serikali wakati mwanasheria mkuu Loretta Lynch anatarajiwa kuhojiwa na kamati ya sheria ya bunge wiki ijayo.

Wabunge walio na hasira wanatarajiwa kumhoji mkurugenzi wa FBI James Comey alhamisi kwa maamuzi yake ya kutopendekeza kushtakiwa Hillary Clinton kwa kutumia barua pepe binafsi kwa matumizi ya serikali wakati alipokuwa waziri wa mambo ya nje ya Marekani.

Comey ameitwa kutoa ushahidi bungeni kwenye kamati ya bunge ya usimamizi wa serikali wakati mwanasheria mkuu Loretta Lynch anatarajiwa kuhojiwa na kamati ya sheria ya bunge wiki ijayo.

Lynch na Comey walikutana Jumatano kabla ya ushahidi wao. Lynch alisema anatafuta mapendekezo ya FBI.

“Nimepokea na kukubali mapendekezo yao kauli moja kwamba uchunguzi wa kina wa mwaka mzima umefungwa na kwamba hakuna mashitaka yatakayofunguliwa kwa watu wowote waliokuwa wametajwa” Lynch alisema katika taarifa yake baada ya kukutana na mkurugenzi wa FBI.

XS
SM
MD
LG