Upatikanaji viungo

Breaking News
Ijumaa, Aprili 26, 2024 Local time: 09:55

Familia zakusanyika Malawi kuwakumbuka na kuwazika waathirika wa Kimbunga Freddy


Waombolezaji wakiwa wamesimama nyuma ya majeneza ya jamaa zao wakati wa mazishi ya halaiki ya waathiriwa wa maporomoko ya udongo katika kambi ya shule ya Msingi ya Naotcha ya Chilobwe mjini Blantyre, Malawi, Machi 15, 2023.AFP
Waombolezaji wakiwa wamesimama nyuma ya majeneza ya jamaa zao wakati wa mazishi ya halaiki ya waathiriwa wa maporomoko ya udongo katika kambi ya shule ya Msingi ya Naotcha ya Chilobwe mjini Blantyre, Malawi, Machi 15, 2023.AFP

Familia za Malawi zilikusanyika siku ya Jumatano kuwakumbuka na kuwazika wathirika wa Kimbunga Freddy huku Rais Lazarus Chakwera akitoa wito kwa jumuiya ya kimataifa kusaidia  huku idadi ya vifo ikiongezeka zaidi.

Freddy ilipiga eneo la kusini mwa Afrika kwa mara ya pili ndani ya mwezi mmoja mwishoni mwa juma na bado ilikuwa ikisababisha mvua kubwa Jumatano, na kutatiza juhudi za kutoa misaada.

Mimi binafsi nimehuzunishwa sana Chakwera aliwaambia waandishi wa habari katika kitongoji cha Chilobwe cha Naotcha, nje kidogo ya mji wa Blantyre. Wakati mwingine unapopita nje na kuona majeneza mengi hivi huwezi kujizuia kutoa machozi kwa sababu wapendwa familia nzima imefutiliwa mbali na wengine wengi ambao wameguswa.

Idara ya usimamizi wa majanga nchini Malawi imesema katika taarifa yake kwamba idadi ya waliofariki kutokana na kimbunga hicho cha pili imeongezeka hadi 225 kutoka 190 huku watu 707 wakijeruhiwa na wengine 41 hawajulikani waliko.

XS
SM
MD
LG