Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumapili, Aprili 27, 2025 Local time: 07:20

Familia ya Chebeya DRC yataka uchunguzi wa kimataifa


Floribert Chebeya kiongozi wa zamani wa kundi la kutetea haki za binadam la Voix des Sans-Voix, VSV huko DRC
Floribert Chebeya kiongozi wa zamani wa kundi la kutetea haki za binadam la Voix des Sans-Voix, VSV huko DRC

Familia ya mwanaharakati wa kutetea haki za binadamu aliyeuwawa mwezi uliopita imeomba kufanyike uchunguzi wa kimataifa baada ya madaktari kutoka Uholanzi kushindwa kujua kilichosababisha kifo chake.

Familia ya mwanaharakati wa kutetea haki za binadamu huko Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo wametoa wito wa kufanyika uchunguzi wa kimataifa kujua sababu za kifo cha ndugu yao Floribert Chebeya.

Tume ya madaktari kutoka Uholanzi na DRC ilitoa ripoti siku ya Alhamisi, inayoeleza kwamba hawajafanikiwa kujua chanzo halisi cha kifo cha mwanaharakati huyo, lakini inasema alifariki kutokana na mshtuko wa moyo. Ripoti hiyo imeongeza utata kutokana na kifo hicho kwani mwili wa Chebeya ulipatikana ndani ya gari lake huku mikono yake ikiwa imefungwa, ikiwa ni siku moja baada ya kukutana na afisa mkuu wa polisi mjini Kinshasa, John Numbi.

Chibalonza Chebeya, dada yake Floribert anasema, kutokana na hali kwamba ripoti mbali mbali za uchunguzi zilizotolewa zinahitilafiana, basi angelipendelea kuwepo na uchunguzi wa kimataifa kwa haraka iwezekanavyo, kwani anaamini kuna uwezekano wa kutoweka kwa ushahdi zaidi. Anasema hajapata kamwe kumsikia kaka yake kuwa na matatizo ya moyo au ugonjwa wa moyo na hivyo hakubaliani kamwe na matokeo ya uchunguzi huo.

Ripoti hiyo ya waatalamu inatofautiana na ile ripoti ya awali iliyotolewa na polisi kwamba kulipatikana mipira ya condom na dawa za kuongeza nguvu maumbile za wanaume ndani ya gari la Chebeya. Serekali ya Kinshasa imehakikisha kwamba kesi ya mwanaharakati huyo itakua ya wazi na ya haki.

XS
SM
MD
LG