Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumapili, Aprili 21, 2024 Local time: 08:43

Miss Kenya 2016 Evelyn Njambi apambana na tohara ya wanawake.


Miss Kenya Evelyne Njambi
Miss Kenya Evelyne Njambi

Evelyn Njambi (Miss Kenya 2016 ) aliingia tano bora kwenye mashindano ya Urembo ya dunia - Miss World yaliofanyika mjini Washington katika ukumbi wa MGM Hotel huko National Harbor mwaka 2016.

Evelyn ameweka historia ya kuwa mshiriki wa kwanza kutoka Afrika mashariki kuingia tano bora ya Miss World.

Yeye ni mtoto wa tatu katika familia ya watoto watano akitokea katika kaunti ya Kiambu ambapo alishinda Miss Kiambu kabla ya kuchukua taji la Miss Kenya 2016 .

Akizungumza na VOA Bi.Njambi anasema alifuatilia mashindano ya urembo tangu akiwa mtoto mdogo na baba yake hakumuunga mkono hapo awali lakini baada ya kushinda taji la Miss Kenya, baba yake aligeuka na kuwa shabiki wake mkubwa pamoja na familia yake yote nao walimpa moyo sana hatimaye kufika hapo alipofika.

Pia anaeleza mafanikio hayaji kirahisi alijiandaa kwa miezi mitatu na alisaidiwa sana na kaunti ya Kiambu pamoja na mkurugenzi wa Ashley Terry Mungai anayeratibu Miss Kenya.

Lengo lake kubwa katika jamii ni kupambana na mila ya tohara kwa wasichana (FGM) kusaidia watoto wa kike nchini humo kuepukana na tohara ya watoto wa kike akisema wengi wao wanakosa kuendelea na masomo.

XS
SM
MD
LG