Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatatu, Aprili 15, 2024 Local time: 00:23

Nini Kinatokea Kwenye Soka ya Uingereza?


UEFA EURO 2016
UEFA EURO 2016

Maswali ambayo washabiki wengi wa soka wa Uingereza wanajiuliza baada ya kipigo cha kushtukiza cha mabao mawili jana dhidi ya timu isiyotarajiwa ya Iceland ni nini kinatokea kwenye soka ya Uingereza? Nini kimefanyika na nini kifanyike?

Sababu tofauti tofauti zinatolewa kutokana na matokeo yaliyoishangaza dunia na haswa waingereza wenyewe lakini ukweli ni kwamba waingereza wanahitaji kuchambua zaidi nini kimetokea na kwa sababu gani.

​Kulikuwa na matatizo ya wachezaji, kwa mfano kiwango kibaya kilichoonyeshwa na kipa Joe Hart, ukosefu wa mabeki wanaoweza kutoa pasi ndefu, mabeki wa pembeni waliokuwa na mtazamo mmoja wa kukimbia kwenye msitari mmoja tu na ukosefu wa winga wa kushoto.

UEFA EURO 2016
UEFA EURO 2016

​Majaribio ya kumchezesha Wayne Rooney kama kiungo wa kati yameonyesha kuwa ni makosa ambayo hayakupaswa kujaribiwa katika mashindano makubwa namna hii.

Uingereza ina kikosi cha kuweza kumfunga Iceland muda wowote ule, kila timu kwenye mashindano haya ina kasoro zake lakini Uingereza ina kiwango cha kuzifunga timu kama Russia, Slovakia na Iceland. Swali ni je kwanini wanashindwa kufanya hivyo? Jibu ni rahisi kuwa Uingereza hawachezi kama timu. Wanacheza kama wachezaji binafsi wasio na mwelekeo na wasiojua wanatakiwa kufanya nini wanapokuwa uwanjani.

Roy Hodgson kocha aliyejitoa wa Uingereza hakuonekana alikuwa na mfumo wowote alioutengeneza kwa wachezaji wake kuufuata.

UEFA EURO 2016
UEFA EURO 2016

​Hakuonyesha kuwa alikuwa na njia inayoeleweka kwa wachezaji wake kuifuata. Raheem Sterling mchezaji mdogo anayeonekana kutokuwa na maamuzi mazuri uwanjani ni mfano mzuri. Hakupewa uwezo na hafundishwi njia sahihi na nini cha kufanya anapokuwa uwanjani.

Hii inaonyesha kwa kiasi kikubwa kwanini timu ya Uingereza ilikuwa ikitegemea zaidi uwezo wa nyota wake na sio kucheza kama timu yenye ushirikiano.

Swali ni je timu ya taifa ya Uingereza inakwenda wapi baada ya hapa?

XS
SM
MD
LG