Waziri mkuu Meles Zenawi amefariki Jumatatu usiku akiwa na umri wa miaka 57 kutokana na ugonjwa usojulikana wakati akipata matibabu katika nchi ya kigeni.
Akizungumza kwenye mkutano na waandishi habari mjini Addis Abeba Jumanne, msemaji wa serikali Bereket Simon hatutoa maelezo zaidi juu ya ugonjwa wa Bw Meles au wapi amekuwa akitibiwa.
Hata hivyo ameleza kwamba waziri mkuu alikua anauguwa tangu mwaka jana na kwamba mkewe na watoto wake walikuwa pamoja nae alipofariki.
"Baada ya wiki kumi za matibabu katika nchi ya kigeni alifariki jana kiasi cha usiku wa manane na mwili wake utarudishwa Etopia hivi karibuni," alisema Bw. Bereket.
Mwili wa Meles ulirudishwa nyumbani Jumanne usiku kutoka Ubelgiji ambako alikuwa anatibiwa
Bereket aliwambia waandishi habari kwamba naibu waziri mkuu na waziri wa mambo ya nchi za nje Hailemariam Desalegn atapishwa kuwa waziri mkuu mpya wa Ethopia. Anasema hapatakuwepo na uchaguzi kwani katiba inamruhusu naibu waziri mkuu kuchukua madaraka.
Akizungumza na Sauti ya Amerika Katibu Mkuu wa zamani wa Umoja wa Afrika Salim Ahmed Salim anasema, Meles atakumbukwa kuwa ni mzalendo aliyetetea maslahi ya Afrika na kuleta mabadiliko makubwa ya kiuchumi na kijami nchini mwake.
Meles Zenawi hakuonekana hadharani tangu mwishoni mwa mwezi wa June. Serikali ya Ethopia ilisuta uvumi kwamba alikuwa katika hali mahtuti.