Upatikanaji viungo

Breaking News
Ijumaa, Machi 29, 2024 Local time: 08:06

Ethiopia yaanza kuzalisha umeme kutoka bwawa lenye utata

Waziri Mkuu Ahmed amesema kuanzia sasa na kuendelea, hakutakuwa na kitu kitakachoizuia Ethiopia.
Waziri Mkuu Ahmed amesema kuanzia sasa na kuendelea, hakutakuwa na kitu kitakachoizuia Ethiopia.

Ethiopia imeanza kuzalisha umeme kutoka kwenye  bwawa la maji lenye utata ambalo linajengwa kwenye Blue Nile.

Ethiopia imeanza kuzalisha umeme kutoka kwenye bwawa la maji lenye utata ambalo linajengwa kwenye Blue Nile.

Hatua hiyo muhimu ilifikiwa Jumapili asubuhi wakati moja ya mitambo 13 ya Bwawa la Grand Renaissance la Ethiopia lilipoanza uzalishaji umeme katika hafla iliyosimamiwa na Waziri Mkuu Abiy Ahmed.

“Kuanzia sasa na kuendelea, hakutakuwa na kitu kitakachoizuia Ethiopia," Abiy alisema.

Bwawa hilo likikamilika litakuwa bwawa kubwa zaidi la kuzalisha umeme barani Afrika.

"Tumeanza tu kuzalisha umeme, lakini hiyo haimaanishi kuwa mradi umekamilika," alisema Kifle Horo, meneja wa mradi wa bwawa hilo. "Itachukua kutoka miaka miwili na nusu hadi mitatu kukamilisha."

Bwawa hilo ambalo litakuwa na jumla ya uwezo wa kuzalisha umeme wa megawati 6,500, limekuwa chanzo cha mvutano kati ya Ethiopia na mataifa mengine yanayotumia maji ya mto Nile, Sudan na Misri.

XS
SM
MD
LG