Macron alitazamiwa kushinda kwa asilimia 57.0-58.5 ya kura ikilinganishwa na Le Pen aliyepata asilimia 41.5-43.0, kulingana na makadirio ya makampuni ya ukusanyaji maoni ya vituo vya televisheni vya Ufaransa kulingana na sampuli ya hesabu ya kura.
Matokeo ni madogo kuliko mchuano wao wa duru ya pili mwaka 2017, wakati wagombea hao wawili walikutana katika duru ya pili na Macron alipata zaidi ya asilimia 66 ya kura.
Kiwango kizuri cha ushindi hata hivyo kitampa Macron kujiamini anapoelekea katika muhula wa pili ya miaka mitano, lakini uchaguzi huo pia umewakilisha kwa jinsi gani mrengo wa kulia umekaribia kutaka kushinda mamlaka nchini Ufaransa.