Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatano, Aprili 17, 2024 Local time: 16:04

Elon Musk akubaliana na Twitter kuhusu ununuzi wa mtandao wake


Mkurugenzi mkuu wa Tesla, Elon Musk
Mkurugenzi mkuu wa Tesla, Elon Musk

Mkurugenzi kwa kampuni ya magari ya Tesla, Elon Musk amekubali kununua mtandao wa kampuni wa Twitter kwa gharama ambayo ilikubaliwa awali ya dola bilioni 44 za kimarekani.

Musk ametoa pendekezo hilo katika barua ambayo kampuni ilifichua kwa tume ya Marekani ya usalama na mabadilishano, hatua ambayo imekuja chini ya kipindi cha wiki mbili kabla ya kesi baina ya pande zote mbili kuanza kusikilizwa katika jimbo la Delawere .

Musk alidai kwamba Twitter ilitoa hesabu ya chini, ya akaunti ghushi kwenye jukwaa lake, huku Twitter kwa upande wake ikishtaki Musk kwa kukiuka makubaliano ya ununuzi. Hata hivyo katika taarifa Twitter ilisema kwamba ilikusudia kukamilisha makubaliano hayo kwa dola 54.20 kwa kila hisa.

Uuzaji wa hisa za Twitter ulisimamishwa kwa muda wakati taarifa hiyo ikisubiriwa. Hata hivyo uuzaji ulirejea tena Jumanne jioni,wakati dhamani ya hisa ikipanda kwa asilimia 22, na kufikia dola 52.

XS
SM
MD
LG