Upatikanaji viungo

Breaking News
Ijumaa, Desemba 08, 2023 Local time: 05:19

Elizabeth Warren atangaza azma ya urais Marekani 2020


Seneta Elizabeth Warren
Seneta Elizabeth Warren

Warren alisema "hata kama tuna tofauti zetu, wengi wetu tunataka kitu hicho hicho. Kuwa na uwezo wa kufanya kazi kwa bidii na kuwahudumia watu tunaowapenda. Hicho ndicho ninachopigania na ndio maana leo ninazindua kamati ya uchunguzi kwa ajili ya kuwania urais”.

Seneta m-democrat Elizabeth Warren wa Marekani ameunda kamati ya uchunguzi kwa ajili ya kuwania urais mwaka 2020. Seneta huyo wa Massachusetts siku ya Jumatatu alikuwa mtu wa kwanza katika kile kilichobashiriwa kutangaza azma yake ya urais ifikapo 2019.

Warren mwenye miaka 69 alizungumza kwenye video iliyotumwa kwa wafuasi wake akisema “hata kama tuna tofauti zetu, wengi wetu tunataka kitu hicho hicho. Kuwa na uwezo wa kufanya kazi kwa bidii na kuwahudumia watu tunaowapenda. Hicho ndicho ninachopigania na ndio maana leo ninazindua kamati ya uchunguzi kwa ajili ya kuwania urais”.

Kamati hiyo inamuwezesha kuchangisha fedha na kujaza nafasi za wafanyakazi kabla ya kuanza rasmi kampeni zake za urais baadae mwaka huu wa 2019.

XS
SM
MD
LG