Upatikanaji viungo

Breaking News
Alhamisi, Aprili 18, 2024 Local time: 08:43
VOA Direct Packages

El Salvador yawahamisha wafungwa 2,000 kwenye jela mpya ili kudhibiti magenge


Baadhi ya wafungwa kutoka makundi ya magenge nchini El Salvador. Picha ya maktaba.
Baadhi ya wafungwa kutoka makundi ya magenge nchini El Salvador. Picha ya maktaba.

Takriban wafungwa 2,000 wengi wao wakiwa washukiwa kutoka kwenye  magenge wamehamishiwa kwenye jela mpya yenye uwezo wa kuwashikilia wafungwa 40,000 nchini El Salvador.

Picha za wafungwa waliokuwa wamenyolewa vichwa, kuchorwa tattoo mwilini, wakiwa bila viatu na wamevaa kaptura nyeupe, zilionyeshwa kwenye mitandao wakati wa zoezi hilo.

Rais wa El Salvador Nayib Bukele ametangaza vita dhidi ya magenge ya wahalifu kwenye taifa hilo la Amerika ya Kati, wakati jela hiyo mpya ikiwa sehemu ya kampeni yake.

Kupitia ujumbe wa Twitter, kiongozi huyo, akielezea kuhusu wafungwa hao amesema, “ haya ndiyo makao yenu mapya na wala hamtaweza kuwadhuru watu tena.”

Hata hivyo makundi ya kutetea haki za binadamu yamepinga kampeni hiyo yakisema kwamba watu wasio na hatia huenda wakalengwa, huku baadhi wakifa hata kabla ya kupata nafasi ya kujitetea. Licha ya hilo, wakazi wengi wa El Salvador wamekaribisha kampeni hiyo.

XS
SM
MD
LG