ECOWAS imeamua pia kutuma ujumbe wa kidiplomasia nchini humo ili kufanya majadiliano na viongozi wapya. Viongozi wa nchi 15 wanachama wa ECOWAS walifanya mkutano wa dharura kwa njia ya mtandao kujadili mzozo wa Guinea Jumatano alasiri.
Baada ya mkutano huo, waziri wa Burkina Faso wa mambo ya nje Alpha Barry, ambaye alishiriki kwenye mkutano huo, alisesema ECOWAS “ iliamua kuisimamisha Guinea kwenye mamlaka zake zote za maamuzi”.
Katika taarifa kwa waandishi wa habari, kwenye mji mkuu wa Burkina Faso Ouagadogou, Barry aliongeza kuwa ECOWAS itaomba Umoja wa Afrika na Umoja wa mataifa kuidhinisha uamuzi wake.
Barry amesema , jumuia hiy pia imeomba jeshi la Guinea kumuachilia huru Conde, na kuanzisha mchakato ambao utaruhusu kurejea kwa uongozi wa kikatiba.Ujumbe wa upatanishi wa ECOWAS unatarajiwa kuwasili Guinea Alhamisi, kulingana na waziri Barry.
Facebook Forum