Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumamosi, Aprili 13, 2024 Local time: 07:13

Ecowas yaipa muda Mali kupanga uchaguzi

Viongozi wa Mali ECOWAS wafanya mkutano wa kipekee mjini Accra.
Viongozi wa Mali ECOWAS wafanya mkutano wa kipekee mjini Accra.

Jumuiya kuu ya kisiasa na kiuchumi ya Afrika Magharibi imesema Ijumaa kuwa itaipa serikali ya mpito ya kijeshi ya Mali miezi 12 hadi 16 kupanga uchaguzi na kuwapa viongozi wa serikali ya kijeshi wa Guinea mwezi mmoja kupendekeza ratiba ya mpito wa kidemokrasia.

Baada ya mkutano wa kilele mjini Accra, viongozi wa Jumuiya ya Kiuchumi ya Afrika Magharibi pia walikubaliana kuwaomba viongozi wa muda wa Burkina Faso kupunguza pendekezo la mpito la miezi 36 hadi muda unaokubalika zaidi, Rais wa tume ya Umoja huo Jean Claude Kassi Brou aliuambia mkutano wa waandishi wa habari.

Afrika Magharibi imekumbwa na mapinduzi mawili nchini Mali, moja nchini Guinea na moja Burkina Faso tangu Agosti 2020, na kuchafua sifa yake kama kielelezo cha maendeleo ya kidemokrasia barani Afrika.

Jumuiya ya mataifa 15 wanachama wa ECOWAS imelaani mara kwa mara mapinduzi hayo na inajaribu kurejesha mamlaka mikononi mwa raia.

XS
SM
MD
LG