Upatikanaji viungo

Breaking News
Alhamisi, Machi 28, 2024 Local time: 11:44

Nchi za Afrika mashariki kujenga bomba la kusafirisha mafuta


Nchi za Afrika mashariki kujenga bomba la kusafirisha mafuta
Nchi za Afrika mashariki kujenga bomba la kusafirisha mafuta

Mataifa matano ya Jumuiya ya Afrika Mashariki-EAC yanafikiria kujenga bomba la kusafirisha mafuta kutoka Uganda kuelekea Rwanda na Burundi, ili kuboresha usalama wa nishati katika eneo hilo.

Afisa mmoja wa cheo cha juu katika wizara ya nishati nchini Kenya, Patrick Nyoike, amesema jumuiya hiyo imepata msaada wa fedha wa dola 600,000 kutoka benki ya maendeleo ya Afrika kwa ajili ya utafiti wa awali.

Nyoike amesema bomba lililopendekezwa litabeba bidhaa za mafuta kutoka kiwanda cha usafishaji mafuta kinachotazamiwa kujengwa Uganda na kingine kilichopo Mombasa nchini Kenya pamoja na masoko ya kimataifa.

Uganda inatarajiwa kuanza uzalishaji wa mafuta mwaka ujao, kufuatia kugundulika kwa mafuta mengi ndani na kuzunguka ziwa Albert, nchini humo.

Nyoike pia alisema EAC imemaliza utafiti juu ya bomba la gesi ya asili lililopendekezwa kutoka Tanzania kuelekea Mombasa. EAC inakadiria hifadhi ya gesi ya asili nchini Tanzania kuwa trilioni 7.5. Afisa huyo wa Kenya alisema vyanzo hivyo vitazuia eneo hilo kutotegemea sana aina moja ya nishati.

XS
SM
MD
LG