Upatikanaji viungo

Breaking News
Ijumaa, Aprili 19, 2024 Local time: 10:34

Duru mpya ya mazungumzo ya Syria yaanza Geneva


Mjumbe maalum wa Umoja wa Mataifa kwa ajili ya Syria Staffan de Mistura akizungumza na waandishi habari mjini Geneva, Uswisi, March 14, 2016.
Mjumbe maalum wa Umoja wa Mataifa kwa ajili ya Syria Staffan de Mistura akizungumza na waandishi habari mjini Geneva, Uswisi, March 14, 2016.

Mwakilishi wa Umoja wa Mataifa kwa ajili ya Syria, Staffan de Mistura, ameanza duru mpya ya mazungumzo ya amani hii leo huko Geneva, akionya kwamba njia mbadala ya mazungumzo ni mbaya zaidi kuliko vita tulivyoshuhudia hadi hivi sasa.

Akizungumza kabla ya kukutana na wajumbe wa serikali ya Syria, de Mistura alisema ni juu ya wa-Syria wenyewe kuamua hali yao ya baadae na Umoja wa Mataifa lazima uwasaidie.

Alisema mpango ni kufanya mazungumzo yasiyo ya moja kwa moja na kila upaande kwa kiasi cha siku 10, kisha baada mapumziko kuitisha duru ya pili wa majadiliano mwanzoni mwa mwezi April na mwingine baada ya hapo. Mwakilishi huyo anasema anaamini utaratibu huu utatayarisha angalau mpango wa kuelekea amani.

XS
SM
MD
LG