Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumanne, Julai 23, 2024 Local time: 13:57

Dunia yakaribisha mwaka wa 2014


Fataki katika mji wa Dubai kuukaribisha mwaka 2014
Fataki katika mji wa Dubai kuukaribisha mwaka 2014
Miji mbalimbali ya dunia ilisherehekea mwanzo wa mwaka mpya wa 2014 kwa fataki na muziki.

Jijini New York takriban watu milioni moja walihimili baridi kali na ulinzi wa hali ya juu katika eneo la Times Square wakisubiri igonge saa sita usiku kuanza rasmi sherehe za kuukaribisha mwaka mpya.

Kwingineko maelfu ya watu waliukaribisha mwaka mpya kwa sherehe na tamasha mbalimbali.

Miji ya Moscow, Dubai, London ilifanya sherehe za mwanzo wa mwaka huku Dubai ikivunja rekodi kwa kuwasha fataki laki nne. Mwaka jana Kuwait iliweka rekodi kwa kuwasha fataki elfu 77.
XS
SM
MD
LG