Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumamosi, Aprili 20, 2024 Local time: 13:34

Dunia yafuatilia kwa karibu sana uchaguzi wa Marekani


Dunia nzima inafuatilia kwa karibu sana matokeo ya uchaguzi mkuu nchini Marekani wenye ushindani mkali sana.

Kuna uwezekano wa kesi kufikishwa mahakamani kupinga matokeo ya uchaguzi huo, hali ambayo inaweza kuchelewesha matokeo rasmi kwa wiki kadhaa.

Baadhi ya wachambuzi wa siasa nchini Marekani, na makundi ya kutetea haki za kiraia yameonya kwamba hatua ya rais Donald Trump kujaribu kujitangaza mshindi wa uchaguzi huo kabla ya mchakato kumalizika ni kinyume cha kanuni za kidemokrasia za Marekani.

Viongozi kadhaa duniani wamesalia kimya, waziri wa mbambo ya nje wa Uingereza Dominic Raab akiambia waandishi wa habari kwamba kila mtu anasubiri kujua matokeo ya uchaguzi huo.

Rais Donald Trump alisema Jumanne usiku kwamba anafikiria kwenda mahakamani kupinga matokeo hayo.

Mnamo mwaka 2000, matokeo ya uchaguzi mkuu yalichelewa kutolewa baada ya kesi kufikishwa mahakamani kujua mshindi wa jimbo la Florida kati ya rais George Bush na mpinzani wake Al Gore. Hatimaye Bush alitangazwa mshindi.

XS
SM
MD
LG