Upatikanaji viungo

Alhamisi, Februari 29, 2024 Local time: 21:53

Dunia yaadhimisha sikukuu ya Krismasi kwa hafla mbalimbali


Krismasi nchini India
Krismasi nchini India

Watu wa tabaka mbalimbali walikusanyika katika maeneo ya ibada Jumamosi kuadhimisha siku ya kuzaliwa kwa Yesu Kristo zaidi ya miaka 2000 iliyopita. Wengine, kwa mujibu wa vyanzo mabalimbali vya habari walihudhuria hafla mbalimbali katika majumba ya starehe na kwingineko kuadhimisha siku hiyo.

Mjini Roma, Italia, kiongozi mkuu wa kanisa Katoliki Papa Francis, alitoa wito kwa jamii na jumuiya ya kimataifa, kuhakikisha kwamba kuna majadiliano kuhusu masuala yanayowakumba.

Katika hotuba yake ya sikukuu ya Krismasi, Papa Francis pia aliwataka viongozi wa ngazi mbalimbali wa kanisa hilo kuendelea kuyajali maslahi ya watu walio na mahitaji katika jamii.

Alisema kwamba Kanisa linapaswa kushughulikia kila aina ya umaskini na kuhubiri injili kwa kila mtu, kwani “sisi sote ni maskini, sisi sote kwa njia moja au nyingine ni wahitaji.”

Nchini Tanzania, Wananchi waliungana na Wakristu wengine duniani kusherehekea sikukuu ya Krisimasi huku katika ibada kwenye makanisa mbalimbali nchini ujumbe kuhusu amani, kuonea huruma wasionacho, kujikinga na ugonjwa wa Corona vikitawala.

Askofu wa Kanisa la KKKT Dayosisi ya Kaskazini Kati, Solomon Massangwa alisema Watanzania wanapaswa kuendelea kuchukua tahadhari kuwa sababu ya janga la Covid -19..

"Kwa Yesu tunajifunza kutoogopa, amekubali kuacha enzi akazaliwa mahali ambapo anaweza kuambukizwa tetanus kwa hiyo hata kama corona ipo ukiwa karibu na Mungu huhitaji kuogopa bali kuchukua tahadhari zote za kujikinga ikiwemo kupata chanjo,” alisema.

Nchini Kenya waumini walihudhuria ibada makanisani huku ujumbe wa amani kwelekea kwa uchaguzi mkuu mwakani ukipewa kipau mbele.

Hali ilikuwa ni hiyo hiyo nchini Uganda, ambako Rais Yoweri Museveni awali alikuwa amewasihi wananchi kuzingatia amani.

Shamrashamra ziliendelea kwingineko duniani huku nchi nyingi zikiripoti, kwa mwaka wa pili mfululizo, kwamba janga la Corona liliathiri maandalizi ya Krismasi.

Ijumaa, waumini wapatao 2000 na viongozi wa dini 200 walihudhuria misa iliyoongozwa na baba mtakatifu kwenye Kanisa la Mtakatifu Peter mjini Rome.

Wale ambao hawakufanikiwa kupata nafasi ya kuingia katika ukumbi wa kanisa hilo waliruhusiwa kushiriki kwa tazama hafla hiyo kwenye skrini kubwa nje ya kanisa hilo.

Idadi ya watu waliohudhuria misa hiyo ilipunguzwa kwa thuluthi moja ya wingi watu kulinganisha na idadi ya watu walioruhusiwa katika miaka ya nyuma hatua hii ni kwa sababu ya janga la COVID-19.

Ilikuwa misa ya pili kama hii ya mkesha wa Krismasi iliyoadhimishwa wakati wa janga la corona. Mwaka jana, takriban watu 200 pekee, wengi wao wakiwa wafanyikazi wa Vatikan, walihudhuria ibada hiyo.

Kwa kawaida waumini na hata wasio waumini wa dini ya Kikristo huadhimisha Krismasi kwa njia mbalimbali, ikiwa ni pamoja na kuzijali jaaa maskini.

XS
SM
MD
LG