Kando na kwamba ni mwaka mpya wa 2020, pia ni mwanzo wa muongo mpya.
Sherehe hizo mjini New York zilifanyika kwenye bustani ya Times Towers ambako mamia ya watu walihesabu dakika pamoja na sekunde kabla ya mwaka mpya kuwadia.
Maelfu wanasemekana kukusanyika kwenye mji mkuu wa Brazil wa Rio de Janeiro ambako fataki zilirushwa huku mziki ukinoga kwenye bandari maarufu ya Copacabana.
Mjini Paris fataki zilirushwa kwenye bustani ya Champs Elysees huku hali ikiwa sawa na hiyo mjini Kremlin, Russia.
Dakika 10 za kurushwa kwa fataki zilirembesha Dubai huku kengele zikipigwa kwenye hekalu za kibudhaa nchini Japan, ikiwa tamaduni iliodumishwa nchini humo kwa muda mrefu.
Imetayarishwa na mwandishi wetu, Washington, DC