Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatano, Aprili 24, 2024 Local time: 08:53

Ndege ya Emirates yazua wasiwasi Dubai


Picha kutoka kwa video yaonesha ndege ya Emirates iliohusika kwenye ajali wakati wa kutua Dubai mapema Jumatano Agosti 3, 2016.
Picha kutoka kwa video yaonesha ndege ya Emirates iliohusika kwenye ajali wakati wa kutua Dubai mapema Jumatano Agosti 3, 2016.

Shirika la ndege la Emirates lenye makao yake Dubai limesema kwamba tukio limetokea mapema Jumatano kwenye uwanja wa ndege wa Dubai.

Shirika la ndege la Emirates lenye makao yake Dubai limesema kwamba tukio limetokea mapema Jumatano kwenye uwanja wa ndege wa Dubai, baada ya moja ya ndege zake kuhusika kwenye ajali wakati wa kutua.

Tukio hilo lilitokea saa saba mchana kwa saa za Dubai likihusisha ndede iliokuwa ikitoka Thiruvananthapuram kusini mwa India. Serikali ya Dubai imesema kuwa abiria wote 275 waliokuwa ndani ya ndege hiyo wameokolewa wakiwa salama.

Watumizi wa mitandao ya kijamii waliweka video kwenye mitandao zikionesha moshi mweusi ukitoka kwenye ndege hiyo.Hata hivyo maafisa wa kampuni hiyo pamoja na wale kutoka uwanjani hapo hawakutoa maelezo zaidi.

Uwanja wa Dubai ndio mkubwa zaidi katika eneo la mashariki ya kati na pia ndio uwanja wa kimataifa wenye shughuli nyingi zaidi ulimwenguni.

XS
SM
MD
LG