Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumamosi, Oktoba 01, 2022 Local time: 07:16

DRC yashutumiwa kwa mauaji ya watu


Raia wa Drc wakiandamana wakati wa uchaguzi mwishoni mwa mwaka jana.

Kwa kuongezea umoja wa mataifa unasema kuwa watu wengine 16 hawajulikani walipo na inatuhumu maafisa kwa kukamata watu kiholela na kuwatesa wakiwa chini ya ulinzi.


Umoja wa mataifa umesema vikosi vya usalama nchini jamhuri ya kidemokrasi ya congo vimeuwa takriban watu 33 katika kipindi cha uchaguzi mwishoni mwa mwaka jana.

Umoja wa mataifa umechapisha ripoti jumanne inayoeleza ukiukwa mkubwa wa haki za binadamu kufuatia uchaguzi wa urais wa novemba mwaka 2011.

Takriban watu 33 wameuwawa na wengine 83 wamejeruhiwa wengi kwa risasi katika mji mkuu wa Kinshasa baina ya novemba 26 na desemba 25. Kwa kuongezea umoja wa mataifa unasema kuwa watu wengine 16 hawajulikani walipo na inatuhumu maafisa kwa kukamata watu kiholela na kuwatesa wakiwa chini ya ulinzi.
Uchunguzi ulifanywa na ofisi ya pamoja ya utetezi wa haki za binadamu ya umoja wa mataifa.

Uchaguzi wa urais na bunge ulifanyika novemba 28. Upigaji kura ulimrejesha joseph kabila katika madaraka lakini uchaguzi ulipingwa kote DRC na jumuiya ya kimataifa hasa kwa upoteaji wa kura na kura kufungamana.

XS
SM
MD
LG