Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumanne, Septemba 17, 2024 Local time: 17:44

DRC yapiga marufuku usafirishaji magogo ili kulinda mazingira


Mfano wa miti inayokatwa kwenye misitu ya Congo
Mfano wa miti inayokatwa kwenye misitu ya Congo

Congo iko chini ya shinikizo la kuimarisha usimamizi wa misitu na kupunguza kasi ya ukataji miti ambayo imeongezeka maradufu katika muongo uliopita, kulingana na takwimu za Umoja wa Mataifa

Waziri wa mazingira wa Jamhuri ya kidemokrasi ya Congo, Eve Bazaiba, alisema Alhamis kwamba nchi hiyo inakusudia kupiga marufuku usafirishaji wote wa magogo na kutekeleza hatua zingine ili kupunguza tishio kwa msitu wake wa kanda ya joto unaovuta hewa ya Carbon ikiwa ni sehemu kubwa dhidi ya mabadiliko ya hali ya hewa.

Makazi ya sehemu kubwa ya msitu wa pili kwa ukubwa duniani, Congo iko chini ya shinikizo la kuimarisha usimamizi wa misitu na kupunguza kasi ya ukataji miti ambayo imeongezeka maradufu katika muongo uliopita, kulingana na takwimu za Umoja wa Mataifa.

Eve Bazaiba alitangaza kusimamishwa kwa usafirishaji wa magogo kwa waandishi wa habari katika mji mkuu Kinshasa lakini hakusema ni lini hatua hiyo itaanza kutekelezwa. "Inaturuhusu sio tu kuwezesha kurudi kwa misitu kwa kawaida lakini pia, program ya upandaji miti ambayo tunayo pamoja na washirika wetu wote wote wa kiufundi, kifedha na maendeleo alisema".

XS
SM
MD
LG