Upatikanaji viungo

Breaking News
Ijumaa, Februari 23, 2024 Local time: 20:41

Kabila awatembelea waathiriwa Sange


Rais wa Jamhuri ya Kidemokrasi ya Congo Joseph Kabila amewatembelea waathiriwa wa ajali ya moto baada ya kuripuka kwa gari la mafuta huko Sange, karibu na mpaka na Burundi.

Rais Joseph Kabila wa DRC alitembelea eneo la ajali ya mripuko wa gari la mafuta, Sange, Kivu ya Kusini, pamoja na kuwatembelea wathiriwa katika hosptali mjini Uvira. Rais anatazamiwa kutembelea pia makaburi ambako wamezikwa kwa pamoja watu walofariki kutokana na ajali hiyo ya moto ulochoma baadhi ya nyumba zilizokua karibu.

Watu 240 wamefariki kutokana na ajali hiyo iliyotokea siku ya Ijumaa na wengine 200 kujeruhiwa, maafisa wa afya wanasema idadi ya vifo huwenda ikaongezeka.

Nyumba zilizoteketea huko Goma Mashariki ya DRC Julai 04 2010.
Nyumba zilizoteketea huko Goma Mashariki ya DRC Julai 04 2010.

Waziri wa afya wa Congo Victore Makwenge, akizungumza na waandishi wa habari baada ya kulitembelea eneo hilo Jumatatu alisema, hiyo ilikua moja kati ya ajali mbaya kabisa ya barabarani katika historia ya Congo. Amesema kuna mahitaji makubwa sana ya madawa, huduma za dharura pamoja na msaada wa kisaikolojia kwa watu waloshuhudia jamaa zao walofariki wengi kwa wakati mmoja.

Bw Makwenge ameahidi kwamba serikali itatowa misaada ya dharura kwa haraka iwezekanavyo ili kuepusha kuongezeka kwa vifo. Rais Kabila alilihutubia taifa siku ya Jumapili na kutoa rambi rambi zake kwa familia za wathiriwa na kutangaza siku mbili za maombolezi ya kitaifa.

Na katika tukiyo jingine Jumapili zaidi ya nyumba 60 ziliteketea katika mji wa Goma kutokana na moto ulotokana na mtu kuacha taa ya mafuta iliyoanguka na kuanzisha moto mkubwa.hakuna habari za idadi ya watu walojeruhiwa na wakazi wa eneo hilo wamelalamika kwamba hakuna afisa wa serikali aliyefika kuwasaidia.

XS
SM
MD
LG