Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumapili, Julai 21, 2024 Local time: 20:38

DRC yafunguwa hifadhi za wanyama Virunga, Solanga


 A baby lowland gorilla rides on his mother's back at the primate sanctuary run by the Cameroon Wildlife Aid Fund in Mefou National Park, just outside the capital Yaounde, March 21, 2009. During the women's Africa Cup of Nations football tournament in Ca
A baby lowland gorilla rides on his mother's back at the primate sanctuary run by the Cameroon Wildlife Aid Fund in Mefou National Park, just outside the capital Yaounde, March 21, 2009. During the women's Africa Cup of Nations football tournament in Ca

Serikali ya Jamhuri ya Kidemokrasi ya Congo (DRC) imesema Ijumma kwamba imeamua kufungua sehemu ya hifadhi za taifa za Virunga na Solanga, ambako ni makazi ya sokwe na wanyama wengi ambao ni nadra, kwa uchimbaji mafuta.

Mapendekezo ya awali ya kuruhusu uchimbaji mafuta katika hifadhi yalipata upinzani mkali sana kutoka kwa wanaharakati wa mazingira, ambao wanasema uchimbaji mafuta utawaweka wanyama pori katika hatari na pia uchimbaji huo utasababisha kuwepo kwa kiwango kikubwa cha carbon dioxide hewani, na kusababisha hali ya joto joto ulimwenguni.

Serikali imetetea haki yake ya kuidhinisha uchimbaji mafuta sehemu yoyote nchini humo na kusema inatilia maanani kuwalinda wanyama na mimea katika maeneo mawili ya makumbusho ya UNESCO.

Baraza la mawaziri limesema katika taarifa yake kwamba wameidhinisha kuundwa kwa tume ya ngazi ya mawazii ambayo itakuwa na jukumu la kutayarisha mipango ya kuyataja maeneo katika hifadhi hizo,ikiwemo kilometa za mraba 1,720 au asilimia 21.5 ya ardhi iliyopo mashariki mwa Congo ilipo hifadhi ya Virunga.

Virunga iko kwenye eneo la msitu lenye volcano huko Afrika ya Kati na ni makazi ya zaidi ya nusu ya idadi ya Sokwe wa milimani waliopo duniani.

Kampuni ya Uingereza ya Soco International ilifanya upimaji wa ardhi katika eneo hilo ili kufahau kama kuna uwezekano wa matetemeko, lakini leseni yake ilikwisha muda wake mwaka 2015.

Hifadhi ya Solanga ina ukumbwa wa kilometa za mraba 33,350 katika bonde la Congo, ambalo lina wanyama wanaojulikana kama tembo wa msituni, sokwe na tausi wa Kongo.

XS
SM
MD
LG