Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumanne, Juni 18, 2024 Local time: 14:45

DRC Yafanya Uchaguzi Disemba 23


Kampeni za uchaguzi DRC 2018
Kampeni za uchaguzi DRC 2018

Jamhuri ya Kidemokrasi ya Congo inafanya uchaguzi mkuu Disemba 23 kuchagua rais na bunge jipya nchini humo pamoja na nafasi mbali mbali za utawala kama magavana wa majimbo na nyinginezo.

Katika ukurasa huu maalum kuhusu uchaguzi huo, tunatupia jicho wagombea wakuu katika nafasi ya rais, wabunge na magavana, maswala muhimu yanayo zungumziwa katika kampeni za uchaguzi ambazo zimeanza tangu mwanzoni mwa mwezi Disemba.

Disemba 23

Baada ya uchelewesho wa takriban miaka miwili, rais Joseph Kabila anaachia madaraka katika jamhuri ya kidemokrasia ya congo baada ya kushikilia uongozi wa nchi hiyo kwa miaka 17.

Rais Joseph Kabila
Rais Joseph Kabila

Wagombea watatu wakuu ambao wanawania nafasi ya kuchukua wadhifa wa urais ni mgombea wa chama tawala Emmanuel Shadary (aliyeteuliwa na Kabila), Martin Fayulu mgombea wa ushirika mmoja wa vyama vya upinzani, na Felix Tshisekedi mgombea wa ushirika mwingine wa vyama vya upinzani, ingawa kuna wagombea wengine 19 wa urais katika uchaguzi huu.

Uchaguzi mkuu wa Congo umekuja baada ya vuta nikuvute ya miaka miwili kufuatilia kumalizika kwa muhula wa pili wa Joseph Kabila mwaka 2014. Kabila aliingia madarakani kwa mara ya kwanza 2001 baada ya kuuawa kwa baba yake Laurent Kabila. Joseph Kabila alichaguliwa kura rais katika uchaguzi mkuu wa 2006 na kuchaguliwa tena kwa awamu ya pili 2011.

please wait

No media source currently available

0:00 0:07:33 0:00

Huu utakuwa uchaguzi wa nne wa kidemokrasia katika historia ya DRC. Wa kwanza ulikuwa baada tu ya nchi hiyo kupata uhuru mwaka 1960.

Shadary anasema alichaguliwa kuwa mgombea katika wadhifa wa urais na rais Joseph Kabila, alikuwa akiueleza umati wa watu katika mkutano wa kampeni.

Lakini Shadary anakabiliwa na ushindani mkali kutoka kwa upinzani ambao umegawanyika lakini una nguvu, akiwemo mtoto wa kiume wa kiongozi wa zamani wa upinzani, marehemu Etienne Tshisekedi.

Felix Tshisekedi, ambaye kwa kiasi kikubwa anaonekana kuwa yuko mbele, aliingia katika kinyang’anyiro mwishoni, baada ya upinzani kumchagua mgombea mwingine kuwa ni mgombea wa ushirika wa upinzani.

Mgombea wa ushirika wa upinzani, ni mfanyabiashara Martin Fayulu, ambaye ameiambia VOA kuwa ana imani kubwa kwamba wapiga kura watamuunga mkono. Hata hivyo, ukusanyaji maoni wa mwezi October uliofanywa na taasisi za kimataifa na zile za ndani ya nchi ulimpa asilimia nane tu ya kura.

Anasema: “Sote tunataka kuyaachamambo mabaya ambayo bwana Kabila alifanya katika nchi hii. Mambo mabaya ambayo kwa miaka 20 kina Kabila wameyafanya katika nchi hii. Rushwa, ukosefu wa usalama, mauaji ya watu wengi. Hayo ndiyo mambo ambayo yanatupa sisi sababu ya kuwa na hamasa, kusudi tusonge mbele na kubadili mambo katika nchi hii.”

Lakini anasema hana uhakika kama uchaguzi huu utampa fursa hiyo na wakati huu, upinzani uliogawanyika unaimba wimbo mmoja wenye ujumbe mmoja, wanaamini kuwa upigaji kura hautakuwa huru na wa haki au wa uwazi.

Andre-Alain Atundu, msemaji wa ushirika wa chama tawala na mshirika wa karibu sana wa Shadary anasema anadhani kuwa muendelezo ni jambo moja muhimu sana, na hilo litaendelea bila ya kujali nani anashinda uchaguzi.

Anasema Shadary ataendelea na nguvu ya maendeleo ile ile ambayo imeanzishwa na Bwana Kabila. “Ukweli ni kwamba, wengine watachukulia fursa ya kile ambacho Bwana Kabila amekiacha. Ni suala la uaminifu. Na kila rais ajaye atataka kuendeleza kila ambaco Bwana Kabila alikuwa na fursa ya kukifanikisha.”

Kwa muda ilionekana kama vile uchaguzi huu hautafanyika huku rais Kabila akidhaniwa anajaribu kung’ng’ania madaraka.

Lakini kufuatia shinikizo kutoka nchi za magharibi, umoja wa Afrika na makundi ya ndani ya nchi hasa kanisa katoliki na mazungumzo yaliyohusisha pande zote tume ya uchaguzi ikatangaza uchaguzi utafanyika Disemba 23.

Tume cha uchaguzi CENI iliandikisha wagombea 21 wa kiti cha urais na takriban wagombea 16,000 kwenye uchaguzi wa bunge wakiwania viti 500 katika bunge la nchi hiyo. Kuna wagombea 20,000 kwenye uchaguzi wa mabunge ya majimbo ambayo yana jumla ya viti 715.

Katumbi na Bemba

Majina mawili makubwa ambayo yalidhaniwa kuwa katika kinyang’anyiro huko yameondolewa. Hao ni Jean-Pierre Bemba aliyewahi kuwa makamu rais nchini humo na Moise Katumbi, wanasiasa waliokuwa na nafasi nzuri lakini wakaondolewa na CENI kwa madai kuwa waliwahi kukutwa na makosa ya jinai katika siku za nyuma.

Katumbi aliyewahi kuwa gavana wa jimbo la Katanga yuko nje ya nchi na hajaruhusiwa kurejea nchini ambako anakabiliwa na mashitaka ya uhaini.

Kulingana na CENI matokeo ya mwanzo ya uchaguzi yanatarajiwa kutolewa Disemba 30, na matokeo kamili rasmi ifikapo Januari 8, 2019. Mshindi wa urais ataapishwa Januari 12, 2019.

XS
SM
MD
LG