Upatikanaji viungo

Breaking News
Alhamisi, Desemba 05, 2024 Local time: 23:08

DRC yadai Rwanda inafadhili waasi wa M23 kwenye jimbo la Kivu Kaskazini


Wanajeshi wa DRC wakiwa mstari wa mbele wa mapambano dhidi ya waasi wa m23.
Wanajeshi wa DRC wakiwa mstari wa mbele wa mapambano dhidi ya waasi wa m23.

Kinshasa kwa mara nyingine Alhamisi imelalamikia janga la kibinadamu, ambalo inasema, linasababishwa na uchokozi wa Rwanda ndani ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, kabla ya mkutano wa Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa kuanza wiki ijayo mjini New York.

Waziri wa mawasiliano Patrick Muyaya na mwenzake wa Sheria Rose Mutombo wametoa malalamishi dhidi ya Kigali wakati wakizungumza na wanahabari mjini Kinshasa. Wamehimiza madai kwamba Rwanda ambayo ni jirani wa Congo upande wa mashariki inaunga mkono waasi wa Kitutsi wa M23, suala ambalo Rwanda imeendelea kukanusha.

Waasi hao wameshika udhibiti wa eneo kubwa kwenye mkoa wa Kivu Kaskazini uliyoko kwenye mpaka kati ya mataifa hayo, tangu kuchukua silaha tena mwishoni mwa 2021, baada ya miaka kadhaa ya utulivu. Muyaya alisema kwamba kuna ushahidi wa kutosha kuwa kuna ukatili unaoendeshwa na jeshi la Rwanda likishirikiana na waasi wa M23.

Wataalam wa UN pia wanalaumu Rwanda kwa kuunga mkono waasi hao, wakati EU hapo Julai ikilalamikia kuwepo kwa wanajeshi wa Rwanda mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo.

Forum

XS
SM
MD
LG