Upatikanaji viungo

Breaking News
Alhamisi, Septemba 28, 2023 Local time: 08:03

DRC wataka Lumbala arejeshwe kutoka Ufaransa


Waasi wa M23 karibu na mpaka wa DRC na Uganda July 2012
Waziri wa Habari wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo - DRC - Lambert Mende anasema serikali ya Rais Joseph Kabila iko tayari kufanya lolote kuhakikisha usalama katika nchi hiyo.

Matamshi hayo yamekuja baada ya Kinshasa kusema Jumapili kuwa itaiomba Ufaransa kumrejesha Kinshasa kiongozi wa upinzani Roger Lumbala kutokana na madai kwamba anaunga mkono waasi wa kundi la M23 mashariki mwa Congo.

Lumbala alitazamiwa kuwasili Ufaransa Jumapili kutokea Afrika Kusini.

Mende alisema serikali ya DRC inataka kumaliza hali ya watu kutoadhibiwa kwa makosa yao kwa sababu wananchi wa Congo wamepata mateso makubwa kutokana na uasi wa M23.

Maafisa wa Burundi walimtia nguvuni Lumbala mapema mwezi huu baada ya kuwasili nchini humo kutokea Rwanda. Aliwekwa katika kizuizi cha nyumbani lakini baadaye aliomba hifadhi ya kisiasa katika ubalozi wa Afrika Kusini.

Mende alisema Jumapili kuwa kokote Lumbala atakakokwenda Kinshasa itamsaka.
XS
SM
MD
LG