Upatikanaji viungo

Breaking News
Ijumaa, Juni 14, 2024 Local time: 18:59

DRC: Ripoti yafichua visa zaidi vya unyanyasaji wa kingono uliotekelezwa na wafanyakazi wa misaada


Mkuu wa WHO Tedros Adhanom Ghebreyesus akizungumza na wahudumu wa afya mjini Beni, DRC.
Mkuu wa WHO Tedros Adhanom Ghebreyesus akizungumza na wahudumu wa afya mjini Beni, DRC.

Wanawake kadhaa wameripoti kudhulumiwa kimapenzi na wafanyakazi wa kutoa msaada kati ya mwaka 2018 na 2020 katika Jamhuri ya kidemokrasia ya Congo.

Afisa mmoja wa ngazi ya juu wa shirika la afya duniani WHO, amesema kwamba wafanyakazi 83 wa kutoa msaada, robo yao wakiwa wafanyakazi walioajiriwa na WHO, walihusika katika kuwahadhaa wanawake kimapenzi, wakati wa mlipuko wa ugonjwa wa Ebola.

Ripoti ya tume huru iliyochunguza sakata hilo imesema kwamba kulikuwepo madai tisa ya ubakaji.

Kati ya madai ya ubakaji ni yaliyotolewa na msichana mwenye umri wa miaka 14 anayeshutumu dereva wa shirika la afya duniani kwa kumbeba kwa gari lake na kumbaka baadaye.

Msichana huyo alijifungua mtoto aliyepata na dereva huyo.

"Ndio, kuna madai ya ubakaji ambayo ni makosa ya uhalifu. Kile ambacho tumefanya ni kuomba kufanyike uchunguzi huru ili kuwafikia waathiriwa na walionusurika ili kupata idhini yao ndipo tuasilishe kesi hizi kwa mamlaka. Tunafanya mazungumzo na mawakili wetu kwa sababu hatujapata ridhaa tunayotaka, na hatua tunazostahili kuchukua baada ya muda kupita," alisema Gaya Gamhewage, kaimu mkurugenzi wa WHO wa kitengo kinachoshughulika na shutuma za manyanyaso ya kingono na ukiukaji wa haki za watu.

Mkuu wa WHO Tedros Adhanom ametoa mpango wa kiutendaji wiki iliyopita akiapa kuhakikisha kwamba Sakata hiyo na waathiriwa, itakuwa kichocheo kikubwa katika kuleta mabadiliko kwa tamaduni za shirika la afya duniani.

WHO limesema pia kwamba litachunguza utepetevu uliofanywa na wakuu wake kuhusiana na Sakata hiyo.

XS
SM
MD
LG