Upatikanaji viungo

Breaking News
Alhamisi, Aprili 18, 2024 Local time: 16:01

Maelfu ya wacongo waondoka Kinshasa


Rais Joseph Kabila wa DRC akipiga kura yake mjini Kinshasa kwenye uchaguzi mkuu uliofanyika Jumatatu, Novemba 28,2011
Rais Joseph Kabila wa DRC akipiga kura yake mjini Kinshasa kwenye uchaguzi mkuu uliofanyika Jumatatu, Novemba 28,2011

Imeelezwa kuwa wakazi wengi wa Kinshasa nchini DRC wanakimbilia nchi jirani kuepuka ghasia za baada ya uchaguzi

Maelfu ya watu wanaukimbia mji mkuu wa Jamhuri ya Kidemokrasi ya Congo-DRC, Kinshasa, wakikhofia kwamba matokeo ya uchaguzi yanayotarajiwa kuitangazwa Jumanne yatazusha ghasia.

Polisi katika nchi ya jirani ya Jamhuri ya Congo wanasema watu wasiopungua 3,000 wamewasili katika mji mkuu Brazzaville, tangu Disemba mbili.

Maafisa wa usalama wanasema wengi wa wanaowasili wanatoka Kinshasa, mji umetenganishwa na mto Congo kutoka Brazzaville, na ambapo hali ni tete.


Maafisa wa uchaguzi nchini DRC wanatarajiwa Jumanne kutangaza matokeo rasmi ya upigaji kura katika uchaguzi mkuu uliofanyika wiki iliyopita.

Matokeo kutoka kiasi cha vituo vya kupigia kura kadhaa, yanaonesha Rais Joseph Kabila anaongoza dhidi ya mpinzani wake mkuu Etienne Tshisekedi, kwa takribani asilimia 49 dhidi ya 34.

Wafuasi kutoka pande zote za Rais Kabila na bwana Tshisekedi wanaonya kwamba ghasia zitazuka kama matokeo hayatatoa ushindi kwa wagombea wao.


Upigaji kura uliofanyika wiki iliyopita ulikuwa uchaguzi pekee huru wa pili kufanyika tangu taifa hilo lililopo Afrika lilipotengana kufuatia miaka kadhaa ya mzozo wa vita ambao ulimalizika mwaka 2003.

Kundi la kutetea haki za binadamu la Human Rights Watch, tayari linaripoti kuuwawa kwa raia wasiopungua 18 na kujeruhiwa kwa watu 100 wengine katika mashambulizi yanayohusiana na uchaguzi.

Upigaji kura uliofanyika zaidi ya siku tatu katika baadhi ya maeneo nchini humo wiki iliyopita, ulielezewa kuwa uligubikwa na ghasia na kile baraza la usalama la Umoja wa Mataifa ulichokiita kuwepo matatizo ya utaratibu wa kujiandikisha na kiufundi.

XS
SM
MD
LG