Upatikanaji viungo

Breaking News
Ijumaa, Juni 14, 2024 Local time: 18:06

Polisi watawanya maandamano kumpinga Kabila DRC


Polisi wametumia nguvu katika miji kadha ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo kutawanyama maandamano ya kupinga Rais Joseph Kabila kuendelea kukaa madarakani baada ya muda wake baadaye mwaka huu.

Watu kadha wametiwa nguvuni na polisi na kuna ripoti za watu kujeruhiwa katika vuta nikuvute na polisi.

Maandamano dhidi ya serikali ya Kabila
Maandamano dhidi ya serikali ya Kabila

​Mamia ya watu walijitokeza katika mji mkuu Kinshasa na miji mingine ya mashariki mwa Congo kama vile Goma, Beni, Butembo, Bunia, Bukavu na Kisangani kupinga hatua ya mahakama ya katiba hivi karibuni kuamua kwamba rais Kabila anaweza kuendelea kuwa madarakani hadi uchaguzi mpya. Uchaguzi ambao ulikuwa ufanyike mwaka huu hauna na dalili na hakuna tarehe ya baadaye iliyotangazwa.

Makundi ya upinzani ndani na nje ya DRC yamepinga vikali uamuzi huo wa mahakama na kuandaa maandamano ya Alhamisi kumwekea shinikizo Rais Kabila afanye uchaguzi mkuu.

Ingawa katika miji mingi maandamano yalianza kwa amani baadaye yaligeuka kuwa na ghasia baada ya polisi kujaribu kutawanya waandamanaji. Serikali ilisema Jumatano kuwa maandamano hayo hayajaruhusiwa.

XS
SM
MD
LG