Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumamosi, Julai 27, 2024 Local time: 04:13

DRC:Mkataba wa amani washindikana


Betrand Bisimwa, kiongozi wa kundi la waasi wa DRC M23.
Betrand Bisimwa, kiongozi wa kundi la waasi wa DRC M23.
Afisa wa uganda amesema serikali ya Jamhuri ya Kidemokrasi ya Congo imekataa kutia saini makubaliano ya amani na kundi la waasi la M23.

Wajumbe wa serikali ya Congo na kundi hilo la waasi walitazamiwa kutia saini makubaliano ya amani katika mji wa Entebbe, Uganda lakini msemaji wa serikali ya Uganda Ofwono Opondo alisema katika ujumbe wake wa twitter kwamba Ujumbe wa serikali ya Congo “umepuuzia jaribio hilo la kutia saini.”

Opondo aliiambia Sauti ya Amerika kuwa wajumbe wa serikali ya Kinshasa walikataa kuingia katika chumba ambako kulikuwa na sherehe za kutia saini makubaliano hayo na kuomba muda zaidi kusoma hati ya makubaliano hayo. Alisema ujumbe huo haukueleza wasiwasi wao ulitokana na nini.

Akizungumza idhaa ya Kiswahili ya Sauti ya Amerika Jumatatu usiku, kiongozi wa kundi la M23 Betrand Bisimwa alisema kundi lake halina nia ya kurejea vitani na limeamua kutumia siasa kufikia malengo yake.

Hata hivyo alilalamika kuwa wajumbe wa serikali walikataa kutia saini mkataba uliofikiwa baada ya mazungumzo ya miezi kumi bila kutoa sababu mahsusi.

Alisema wawakilishi wa serikali ya Kinshasa walisema wanataka kubadilisha mkataba huo na kuonya kuwa ikiwa serikali haitaki kutia saini makubaliano ya amani na kundi hilo, itakuwa inatafuta vita na Wacongomani.
XS
SM
MD
LG