Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatatu, Februari 26, 2024 Local time: 10:52

Rais Kabila asema ushindi wake halali


Rais Kabila asema ushindi wake halali
Rais Kabila asema ushindi wake halali

Rais Kabila wa DRC amewaambia waandishi wa habari mjni Kinshasa kuwa amechaguliwa kihalali

Rais wa Jamhuri ya Kidemokrasi ya Congo, Joseph Kabila anasema hakuna wasi wasi wowote kwamba kuchaguliwa kwake katika uchaguzi mkuu uliofanyika mwezi uliopita ni halali.

Katika mkutano na waandishi wa habari mjini Kinshasa, Jumatatu, Kabila alikanusha matamshi ya taasisi ya Carter Centre kwamba uchaguzi wa mwezi uliopita ulisimamiwa vibaya na kulikuwa na mapungufu mengine ya kimsingi.

Taasisi hiyo inayoangalia masuala ya uchaguzi yenye makao yake nchini Marekani ilisema Jumamosi kwamba vituo vya kupigia kura katika eneo la wafuasi wa Kabila viliripotiwa watu kujitokeza kwa wingi na kwamba kura nyingi katika maeneo ya mpinzani wake ziliripotiwa kuibiwa.

Ijumaa tume ya uchaguzi nchini DRC ilimtangaza bwana Kabila mshindi wa uchaguzi huo. Mpinzani wake Etienne Tshisekedi aliyapinga matokeo hayo na alijitangaza mwenyewe kuwa ni Rais.

Rais Kabila, Jumatatu alikanusha kuwa kuna matatizo nchini Congo na alimtaka bwana Tshisekedi kwa maneno yake Rais kabila “ tumia busara njema kwa kufuata mfumo wa sheria”, kama hakubaliani na matokeo ya uchaguzi.

Ghasia za waandamanaji na wizi wa mali umesababisha vifo vya watu wane mjini Kinshasa kufuatia kutangazwa kwa matokeo ya uchaguzi, lakini polisi wengi wa kutuliza ghasia na wale waliowekwa mitaani wameweza kurejesha hali ya utulivu katika mji.

Bwana Tshisekedi anawataka wafuasi wake kuwa watulivu na kusubiri maelekezo zaidi. Pia ameelezea matumaini kuwa jumuiya ya kimataifa itasaidia kuzungumzia mzozo uliopo.

Kura za urais na wabunge zilizopigwa wiki mbili zilizopita, ulikuwa ni uchaguzi wa pili huru tangu taifa hilo lililopo Afrika lilipoachana na miaka kadhaa ya vita vya wenyewe kwa wenyewe ambavyo vilimalizika mwaka 2003.

XS
SM
MD
LG