Vyama vya siasa nchini Jamhuri ya Kidemokrasi ya Congo (DRC) vimefikia makubaliano katika mkesha wa mwaka mpya, kwa kumtaka rais wa nchi hiyo kuachia madaraka baada ya uchaguzi ambao lazima ufanyike mwisho wa mwaka huu wa 2017.
Chama tawala awali kilipendekeza kwamba Joseph Kabila aondoke madarakani baada ya uchaguzi utakaofanyika katikati ya mwaka 2018.
Mkataba uliofikiwa unamaliza miezi kadhaa ya vurugu, huku dazeni ya watu wakiwa wameuawa na mamia kukamatwa, juu ya vipi na lini Kabila ataondoka madarakani baada ya miaka 15 akiwa katika hatamu za uongozi katika taifa hilo la Afrika ya kati.
Umoja wa Mataifa umeyasihi majeshi ya Congo kujizuia kutumia nguvu na kuruhusu waandamanaji wa upinzani kutoa sauti zao za upinzani.