Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumanne, Septemba 17, 2024 Local time: 04:14

Serikali na Upinzani DRC wafikia makubaliano


Maaskofu wa kanisa katoliki wakisali katika uzinduzi wa mjadala wa kisiasa mjini Kinshasa, DRC. Desemba 8, 2016.
Maaskofu wa kanisa katoliki wakisali katika uzinduzi wa mjadala wa kisiasa mjini Kinshasa, DRC. Desemba 8, 2016.

Mkataba rasmi utasainiwa Jumamosi, na nafasi ya waziri mkuu itashikiliwa na umoja wa upinzani wa Rassemblement.

Serikali ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC) na vyama vya upinzani vimefikia muafaka juu ya mkataba wa kisiasa ambao utamaliza mgogoro uliokuwa unaendelea nchini humo.

Mwandishi wa idhaa ya Kiswahili VOA nchini DRC, Salehe Mwanamilongo amesema pande zote mbili zimekubaliana katika vipengele vyote vya mkataba huo likiwemo suala la kugawana madaraka ambapo muungano wa Rassemblement umepewa nafasi ya waziri mkuu.

Hata hivyo macho na masikio ya raia wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo sasa yanasubiri kwa hamu mchakato wa kusaini mkataba huo ambao umepangwa kufanyika Jumamosi.

Kwa mujibu wa Felix Tshisekedi anaye ongoza ujumbe wa kambi ya upinzani alikiri kuwa pande zote ziliridhishwa na hatua ziliofikiwa katika mazungumzo hayo.

Japokuwa alikuwa na wasiwasi kuwa kulikuwa na ishara za kuwepo na tofauti baina ya pande mbili, alisema katika ujumbe wake wa twitter.

Kwa mujibu wa duru za siasa maaskofu wa Kanisa Katoliki (CENCO) waliendesha juhudi za mwisho za upatanishi kwa kukutana na Etienne Tshisekedi wa upande wa upinzani na Rais Joseph Kabila kwa ajili ya kuwapa mapendekezo ya mwisho ya mkataba wa kisiasa.

Kwa upande wake mashirika ya kiraia yaliomba kuweko na mtizamo mpya wa wanasiasa kwa ajili ya kunusuru utaratibu wa uchaguzi na hasa kuepuka umwagikaji wa damu.

Kwa hiyo mashirika hayo yalipendekeza kuwepo na mgawanyo wa madaraka kwenye nyanja za kisiasa.

Valentin Vangu, mratibu wa mashirika ya kiraia kwenye jimbo la Kongo ya kati amesema kwamba hatua ya kugawana madaraka inaweza kupunguza uhasama ulioko hivi sasa.

XS
SM
MD
LG