Upatikanaji viungo

Breaking News
Alhamisi, Machi 28, 2024 Local time: 14:42

Tume ya uchaguzi DRC yahusishwa na kadhia ya rushwa


Baadhi ya wananchi wa DRC wakiandamana kupinga kuakhirishwa kwa uchaguzi mkuu mpaka 2018.
Baadhi ya wananchi wa DRC wakiandamana kupinga kuakhirishwa kwa uchaguzi mkuu mpaka 2018.

Gazeti moja la Ubelgiji limechapisha ripoti wiki iliyopita likisema kuwa tume ya uchaguzi ya Congo imelipwa takriban dola milioni 2.4 kama ada kwa benki zenye uhusiano na rais wa DRC, Joseph Kabila.

Gazeti hilo pia limesema tume hiyo ilitoa kiasi cha dola milioni 7.5 fedha taslimu kutoka benki ya BFGI, kwa sababu ambazo haziko bayana. Madai hayo yanahusishwa na mkopo wa dola bilioni 25 ambao benki uliuotoa kwa tume hiyo ya uchaguzi inayojulikana kama CENI.

Uchaguzi wa DRC ulitarajiwa kufanyika mwezi huu, lakini umeakhirishwa mpaka Aprili 2018. Serikali imedai kwamba ukosefu wa rasilimali za kifedha unaoikumba CENI ni moja ya sababu kuu kuhusiana na uchelewesho huo.

Rais wa shirika la kisheria la Congo, Georges Kapiamba ameiambia VOA kuwa ugunduzi huo unatia wasi wasi mkubwa hasa kutokana rasilimali ambazo wamepewa CENI na kwasababu tume ya uchaguzi ilijidai kuwa haitaweza kuandaa uchaguzi kulingana muda uliowekwa kikatiba kwa misingi kuwa haikuwa na fedha za kutosha.

Kapiamba amemuandikia mwanasheria mkuu wa Congo akimtaka kuchunguza suala hili. Lakini hatarajii kuwa ombi lake litashughulikiwa.

Kulinga na ujuzi wetu katika siku zilizopita, Kapiamba amesema, hawana imani kuwa mwanasheria mkuu anaweza kutekeleza hilo kwa uhuru kama ambavyo tungependa. Kapiambia anadai kuwa wale wenye rasilimali au wale ambao wako kwenye chama tawala wanaweza kulindwa kwa chochote kile ambacho wanakifanya au vitenda vyao.

Serikali ya Ubelgiji pia imetaka uchunguzi kamili ufanywe.

Kwa mujibu wa benki, ada hizi si za kawaida kupewa kiwango hiki cha mkopo, wakati rais wa CENI amedai kwamba kutoa fedha taslimu kutoka katika benki ilikuwa ni kwa ajili ya malipo ya mishahara, kukodi magari na kununua mafuta katika sehemu za ndani za nchi ambako hakuna huduma za benki.

Ugunduzi huo umevutia mtizamo wa ziada kwasababu kaka wa kambo wa Kabila ni mkuu wa BFGI na moja ya dada zake rais aliorodheshwa kuwa mmiliki wa asilimia 40 katika benki kuanzia Oktoba 2014.

Shutuma hizi, ni chanzo cha nyaraka ambazo zimepelekwa kwenye vyombo vya habari na mfanyakazi wa zamani wa BFGI, na pia zilimlenga Albert Yuma, rais wa Gecamines, kampuni ya taifa ya uchimbaji madini, na mshirika wa karibu wa Kabila.

XS
SM
MD
LG