Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumapili, Aprili 21, 2024 Local time: 09:11

Mapigano yasababisha wimbi la wakimbizi DRC


Jenerali Bosco Ntaganda
Jenerali Bosco Ntaganda

Wakazi katika maeneo yaliyokumbwa na vita uhama nyumba zao wakati wa usiku na kuelekea maeneo jirani yaliyo salama

Hali ya usalama katika jimbo la Kivu Kaskazini, Jamhuri ya Kidemokrasi ya Congo imezidi kuwa ya wasiwasi kufuatia ongezeko la wimbi la wakimbizi wanaokimbia mapigano kati ya jeshi la serikali na waasi wa kundi la Bosco Ntaganda.

Mapigano haya yamesababisha wakimbizi wengi kuvuka mpaka kupitia mji wa Goma na kuingia Gisenyi nchini Rwanda. Mapigano haya yamesababisha jeshi la serikali kupoteza kambi yake muhimu ya Mushake iliyopo kilometa 50 magharibi mwa Mji wa Goma.Serikali ya Mkoa wa kivu kaskazi imewaomba raia wake kubaki kuwa watulivu kwani mji wa Goma bado upo mikononi mwa jeshi la serikali na imewaomba askari hao waasi kujiunga na jeshi la serikali ili kuendeleza ujenzi wa amani.

Akielezea sababu za kukimbia makazi yao mmoja wa wakazi wa wilaya ya Masisi anasema “Tulitoka saa saba usiku na mpaka sasa hivi ndio tunafika Goma, Masisi hali ya wasi wasi ilianza saa kumi na mbili jioni hadi saa saba usiku na sisi tukaanza kutoka pole pole,” wengine walisema “tunakimbia vita sie tulitoka Sake saa nane usiku na tumekuja kwa miguu nipo na watoto wamebakia nyuma”

Baadhi ya watoto wameathirika katika mapigano haya ambapo wengi wao hutembea mwendo wa safari ndefu kwa miguu na hatimaye hupotea na kutengana na wazazi au familia zao.

XS
SM
MD
LG