Upatikanaji viungo

Breaking News
Alhamisi, Mei 30, 2024 Local time: 22:23

DRC: EU yamchukulia vikwazo msemaji wa M23


Bendera za Umoja wa Ulaya nje ya makao makuu ya EU, mjini Brussels.
Bendera za Umoja wa Ulaya nje ya makao makuu ya EU, mjini Brussels.

Umoja wa Ulaya umesema umeongeza watu wengine nane katika orodha yake ya vikwazo kuhusiana na mzozo wa DRC, ikiwemo viongozi wa waasi na mfanyabiashara raia wa Ubelgiji.

Imeongeza vikwazo vyake dhidi ya watu 10 hadi desemba 2023. Kwa mujibu wa taarifa kutoka baraza la Ulaya, vikwazo hivyo ni pamoja na kuzuiwa mali , na marufuku ya kuingia Ulaya . Walioko kwenye orodha mpya ni Willy Ngoma, msemaji wa kundi la M23 ambalo limekuwa likipigana na jeshi la Congo upande wa mashariki, na Alan Goetz mfanyabiashara wa Ubelgiji.

Ngoma hakujibu alipotakiwa kutoa maoni yake.

Goetz alituma taarifa kwa shirika la habari la Reuters akisema kujumuishwa kwake kwenye orodha hakuna sababu na kuiomba EU kubatilisha azimio lake.

EU imesema Goetz alikuwa mmiliki wa faida na mkurugenzi mkuu wa zamani wa kampuni ya madini iliyosajiliwa Uganda ambayo inapata faida kutokana na madini yanayodhibitiwa na makundi ya wanamgambo katika jimbo la Kivu Kaskazini.

XS
SM
MD
LG