Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatatu, Oktoba 07, 2024 Local time: 22:54

Ajali ya ndege DRC yauwa watu watatu


Ndege za aina ya Antonov hutumiwa zaidi kwa usafiri DRC
Ndege za aina ya Antonov hutumiwa zaidi kwa usafiri DRC

Augustin Katumba Mwanke ni miongoni mwa waliokufa katika ajali iliyotokea Bukavu

Ajali ya ndege huko mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasi ya Congo-DRC, imeuwa watu watatu akiwemo mshauri wa karibu wa Rais Joseph Kabila.

Augustin Katumba Mwanke alikufa akiwa ndani ya ndege binafsi ilipopata ajali kwenye njia ya kuondoka uwanja wa ndege wa Bukavu. Rubani na msaidizi wake pia walikufa katika ajali hiyo.

Mwanke alitambulika kama mshirika wa karibu katika utawala wa Rais Kabila na alikuwa na ushawishi mkubwa. Ajali hiyo pia iliwajeruhi vibaya watu wanne, akiwemo waziri wa fedha, Matata Ponyo na gavana wa jimbo la Kivu Kusini, Marcellin Cishambo.

Waziri wa habari nchini DRC, Lambert Mende, ameiambia Sauti ya Amerika-VOA kwamba majeruhi watapelekwa nchini Afrika kusini kwa matibabu Jumatatu. Maafisa wa usalama wanachunguza chanzo cha ajali hiyo.

Ajali za ndege zinatokea mara kwa mara nchini DRC, nchi ambayo ina rekodi mbaya duniani katika masuala ya usalama wa anga.

XS
SM
MD
LG