Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatano, Julai 24, 2024 Local time: 22:15

Mkuu wa Tume ya Uchaguzi DRC ajiuzulu


Ndege ya CENI ikiwa imebeba maboksi ya kura kupeleka Lubumbashi, DRC (novemba 2011)
Ndege ya CENI ikiwa imebeba maboksi ya kura kupeleka Lubumbashi, DRC (novemba 2011)

Kiongozi wa tume huru ya uchaguzi (CENI) nchini Jamhuri ya Kidemokrasi ya Congo, Padri Apolinaire Malumalu Muhongolo amejiuzulu wadhifa wake kutokana na hali yake ya kiafya ambayo haimruhusu kuendelea tena na shughuli za tume hiyo kwa ufanisi.

Bw. Muholongo katika kipindi cha uongozi wake katika CENI mara kadhaa amekuwa akisumbuliwa na maradhi na alishawahi kwenda Afrika Kusini na Marekani kwa matibabu ambapo pia alifanyiwa upasuaji kwa matatizo ya kichwa.

please wait

No media source currently available

0:00 0:03:02 0:00
Kiungo cha moja kwa moja

Lakini kwa mujibu wa vyanzo mbalimbali nchini DRC inadaiwa kuwa Bw. Muholongo huenda amejiuzulu kutokana na shinikizo la kisiasa.

Kiongozi wa chama cha upinzani cha UPDS cha Etienne Tshisekedi, Ribesi Mikindo, anadai kuwa Bw. Muholongo hakuwa akifanya shughuli zozote katika CENI na hivyo ni vyema apatikane mtu mwingine wa kuchukua wadhifa wake.

Lakini chama tawala cha Rais Joseph Kabila cha PPRD kinadai hakuna shinikizo la kisiasa ambalo limemfanya kiongozi wa CENI kijiuzulu. Akizungumza na VOA mkuu wa PPRD, Norbert Asogya anasema tatizo la afya ndiyo limemfanya Bw. Muholongo kufanya maamuzi ya kuachia uongozi na hivyo kupisha wengine waendelee na kazi.

Lakini baadhi ya wanawake katika mji wa Butembo wamesikitishwa na maamuzi ya kiongozi wa CENI, na hivyo kuzisihi taasisi husika kufanya juhudi za ziada za haraka kumpata kiongozi atakayechukua nafasi ya Bw. Muholongo.

XS
SM
MD
LG